Maneno ya Msingi: Nomino, Vitenzi, Vivumishi na Vielezi
Nomino
Nomino za Globasa hazitofautishi kati ya umoja na wingi.
- maux - panya (umoja), panya (wingi)
- kalamu - kalamu (umoja), kalamu (wingi)
Nomino za Globasa hazina viambishi tamati vya uanishi au ukanushi (mfano 'the' or 'a' kwa Kiingereza).
- janela - dirisha, madirisha
Ikiwa ni muhimu kusisitiza uanishi, hin (huyu/hawa/hii/hizi) au den (yule/wale/ile/zile) zinaweza kutumika.
- hin kitabu - kitabu hiki, vitabu hivi
- den flura - ua lile, maua yale
Ikiwa ni muhimu kusisitiza umoja, un (moja) inaweza kutumika.
- un denta - jino moja
- hin un denta - jino hili (moja)
Ikiwa ni muhimu kusisitiza wingi, plu (nyingi) inaweza kutumika.
- plu pingo - matofaa (nyingi), matofaa
- den plu pingo - matofaa yale (nyingi)
Jinsia
Katika Globasa, nomino zinazoashiria watu na wanyama kwa kawaida hazina jinsia.
- ixu - mtu mzima (mwanamume, mwanamke)
- nini - mtoto (mvulana, msichana)
- gami - mwenzi (mume, mke)
- mumu - ng'ombe (dume, jike)
Ikiwa ni muhimu kusisitiza jinsia, vivumishi fem (jike/wa kike) na man (dume/wa kiume) vinaweza kutumika kama viambishi awali.
- femnini - msichana; mannini - mvulana
- femixu - mwanamke; manixu - mwanamume
- femgami - mke; mangami - mume
- femmumu - ng'ombe jike; manmumu - ng'ombe dume
Asili ya neno fem: Kiingereza (feminine), Kifaransa (féminin), Kijerumani (feminin), Kihispania (femenina)
Asili ya neno man: Kimandarini (男 “nán”), Kifaransa (masculin), Kihispania (masculino), Kiingereza (masculine), Kijerumani (männlich), Kihindi (मर्दाना “mardana”), Kiajemi (مردانه “mardane”)
Nomino chache zinazoashiria watu huonyesha jinsia.
- matre au mama - mama
- patre au papa - baba
Kumbuka: Neno lisilo na jinsia kwa mzazi/wazazi ni atre. Neno lisilo na jinsia kwa mama/baba ni mapa.
Nomino katika Vishazi vya Mwanzo wa Sentensi
Fe mara nyingi hutumika katika vishazi vya mwanzo wa sentensi vyenye nomino.
- Fe fato, - Kwa kweli
- Fe fini, - Mwishowe
- Fe bonxanse, - Kwa bahati nzuri
- Fe asif, - Kwa bahati mbaya, Kwa masikitiko
- Fe onxala, - Kwa matumaini
- Fe folo, - Kwa hiyo
- Fe misal, - Kwa mfano
- Fe xugwan, - Kwa kawaida
- Fe benji, - Kimsingi
- Fe durama, - Wakati mwingine
- Fe rimara, - Tena
- Fe moy kaso, - Kwa vyovyote vile
- Fe alo kaso, - Vinginevyo
- Fe nunya, - Kwa sasa, Sasa
- Fe leya, - Hapo awali, Zamani
- Fe xaya, - Baadaye, Katika siku zijazo
Uambatanisho
Katika Globasa, nomino inaweza kufuatwa na nomino nyingine bila kutumia kihusishi wakati nomino ya pili inabainisha utambulisho wa nomino ya kwanza. Hii inajulikana kama uambatanisho.
- Hotel Kaliforni - Hoteli ya California
- Estato Florida - Jimbo la Florida
- Towa Babel - Mnara wa Babeli
- Dolo Onxala - Mtaa wa Matumaini
- Myaw Felix - Paka Felix
- misu doste Mark - rafiki yangu Mark
- lexi kursi - neno kiti
Kipande di: Maneno Maalum ya Kitamaduni na Majina Maalum
Kipande di kinaweza kutumika kwa hiari kuashiria maneno maalum ya kitamaduni na majina maalum ambayo yana umbo sawa na maneno ya kawaida ambayo tayari yameanzishwa katika Globasa.
- soho - ya pande mbili, -a kuheshimiana
- (di) Soho - Soho (eneo la Jiji la New York)
Kipande ci: Upendo na Mapenzi
Nomino au jina maalum linaweza kufuatwa na kipande ci kuashiria upendo au mapenzi.
- mama - mama
- mama ci - mama mpendwa (kwa lafudhi ya mapenzi)
- nini - mtoto
- nini ci - mtoto mpendwa (kwa lafudhi ya mapenzi)
- Jon - John
- Jon ci - Johnny
Maneno ya Heshima: Gao na Kef
Kivumishi gao (juu, -refu) na nomino kef (bosi, chifu) zinaweza kutumika kama maneno ya heshima.
- alimyen - mwalimu
- gao alimyen - mwalimu mkuu/mwalimu mwenye uzoefu mkubwa (sawa na "master" kwa kingereza)
- papa - baba
- kef papa - bosi
Nomino/Vitenzi
Katika Globasa, nomino/vitenzi ni maneno ambayo yanaweza kufanya kazi kama nomino au kitenzi.
- ergo - kazi (nomino au kitenzi)
- danse - dansi (nomino au kitenzi)
- yam - mlo (nomino) au kula (kitenzi)
- lala - wimbo (nomino) au kuimba (kitenzi)
Ulinganisho wa Nomino/Vitenzi
Ulinganisho wa nomino/vitenzi huonyeshwa kama ifuatavyo kwa kutumia maneno max (zaidi), min (chini, -chache), dennumer (idadi ile ile, nyingi kama), denkwanti (kiasi kile kile, -ingi kama), kom (kama, kuliko).
Kwa nomino:
- max... kom... - ...zaidi... kuliko...
- min... kom... - ...chache... kuliko...
Mi hare max kitabu kom yu.
Nina vitabu vingi kuliko wewe.
Yu hare min kitabu kom mi.
Una vitabu vichache kuliko mimi.
- max te/to kom... - vingi/kingi (vyake) kuliko...
- min te/to kom... - vichache/kichache (vyake) kuliko...
Mi hare max to kom yu.
Nina vingi (vyake) kuliko wewe.
Yu hare min to kom mi.
Una vichache (vyake) kuliko mimi.
- max kom - zaidi ya
- min kom - chini ya
Mi hare max kom cen kitabu.
Nina vitabu zaidi ya mia moja.
Yu hare min kom cen kitabu.
Una vitabu chini ya mia moja.
- dennumer... kom... - ...nyingi kama...
Te hare dennumer kitabu kom mi.
Ana vitabu vingi kama mimi.
- dennumer te/to kom... vingi (vyake) kama...
Te hare dennumer to kom mi.
Ana vingi (vyake) kama mimi.
- denkwanti... kom... ...-ingi kama...
Yu yam denkwanti risi kom mi.
Unakula mchele mwingi kama mimi.
- denkwanti to kom... ...-ingi (chake) kama...
Yu yam denkwanti to kom mi.
Unakula kingi (chake) kama mimi.
Kwa vitenzi:
- max... kom.... au max kom... - zaidi ya
Myaw max somno kom bwaw.
au: Myaw somno max kom bwaw.
Paka hulala zaidi
ya mbwa.
- min... kom.... au min kom... - chini ya
Bwaw min somno kom myaw.
au: Bwaw somno min kom myaw.
Mbwa hulala chini
ya paka.
- denkwanti... kom... au denkwanti kom... - ...-ingi kama
Bebe denkwanti somno kom myaw.
au: Bebe somno denkwanti kom myaw.
Mtoto
hulala -ingi kama paka.
Ili kuonyesha kadiri... ndivyo..., Globasa hutumia folki... max/min, max/min.
Folki mi max doxo, mi max jixi.
Kadiri ninavyosoma zaidi, ndivyo ninavyojua zaidi.
Mpangilio wa vishazi hivi unaweza kubadilika:
Mi max jixi, folki mi max doxo.
Ninajua zaidi, kadiri ninavyosoma zaidi.
Aina za Vitenzi
Vitenzi vinafafanuliwa katika kamusi kama vitenzi visaidizi, vitenzi vihusishi, vitenzi elekezi, vitenzi sielekezi, au vitenzi elekezi na sielekezi (ambitransitive). Viambishi tamati vinavyoonekana katika sehemu hii (-cu, -gi, -ne, -do, -pul) vimeelezwa chini ya Viambishi Vya Kawaida hapo chini. Kiambishi awali xor- kimeelezwa chini ya Uundaji wa Maneno: Viambishi Awali.
Vitenzi Visaidizi
Vitenzi visaidizi hufuatwa mara moja na kitenzi kingine, ambacho kinaweza kuachwa. Kuna vitenzi visaidizi vitatu tu katika Globasa: abil (weza), ingay (faa, paswa), musi (lazima).
Vitenzi Vihusishi
Vitenzi vihusishi huunganisha kiima na kijalizo chake. Kwa sasa kuna vitenzi vihusishi 12: sen (kuwa), xorsen (kuwa, anza kuwa), sencu (kuwa), sengi (sababisha kuwa), kwasisen (onekana kama), okocu (tazama/onekana), orecu (sikia/sikika), nasacu (nusa/nukia), xetocu (onja/ ladha), pifucu (gusa/gusika), hisicu (jisikia kimwili au kihisia), ganjoncu (jisikia kihisia).
Vitenzi Elekezi
Vitenzi elekezi huchukua yambwa tendewa: haja (hitaji), bujo (kamata), gibe (toa). Hata hivyo, vitenzi elekezi vingine wakati mwingine au mara nyingi huacha yambwa tendewa: doxo (soma), yam (kula), lala (imba), nk.
Baadhi ya vitenzi elekezi mara nyingi au karibu kila mara hutumiwa bila yambwa tendewa: somno (lala), haha (cheka), pawbu (kimbia), fley (ruka), n.k. Haya yanajulikana katika Globasa kama vitenzi elekezi vya yambwa mwangwi kwa kuwa yambwa tendewa ya hiari ni neno lile lile kama kitenzi.
Mi le somno (lungo somno).
Nililala (usingizi mrefu).
Yu le haha (sotipul haha).
Ulicheka (kicheko kikubwa).
Kiambishi tamati -gi kinaweza kutumika kwa vitenzi elekezi kwa maana ya kusababisha (yambwa tendewa) ku[kitenzi mzizi], kufanya (yambwa tendewa) [kitenzi mzizi].
Kam yu fleygi hawanavi?
Je, unarusha ndege?
Mi xa sampogi bwaw fe axam.
Nitamtamabeza mbwa jioni.
Payaco le hahagi mi.
Mchekeshaji alinifanya nicheke.
Vitenzi Sielekezi
Vitenzi sielekezi havichukui yambwa tendewa: idi (enda), konduta (jiendesha, kuwa na tabia), loka (kuwa mahali fulani), side (keti), garaku (zama). Vitenzi sielekezi vinaweza kubadilishwa kuwa vitenzi elekezi kwa matumizi ya hiari ya -gi vikiwa na yambwa tendewa.
- garaku - zama
garaku(gi) - (sababisha) kuzama
Navikef le garaku.
Nahodha alizama.
Navikef le garaku(gi) navi.
Nahodha aliizamisha meli.
Katika unyambulishaji wa maneno, hata hivyo, -gi ni lazima. Linganisha vivumishi vifuatavyo vilivyonyambuliwa na garaku na kiambishi tamati -ne.
garakune navikef - nahodha anayezama
garakugine navikef- nahodha anayeizamisha (meli)
Vitenzi Elekezi na Sielekezi (Ambitransitive Verbs)
Vitenzi elekezi na sielekezi (ambitransitive verbs) katika Globasa ni vitenzi ambavyo kiima cha maana isiyoelekeza na yambwa tendewa ya maana elekezi hupitia kitendo/hali ile ile ya kitenzi. Maana isiyoelekeza ya vitenzi hivi inaweza kutumia kwa hiari -cu na maana elekezi inaweza kutumia kwa hiari -gi.
Kuna aina ndogo nne za vitenzi elekezi na sielekezi: vitenzi vya hisia, vitenzi vya hali, vitenzi visivyo na mtendaji, na vitenzi vya mkao/mahali au mwendo.
Vitenzi vya Hisia
Vitenzi elekezi na sielekezi vinavyoashiria hisia vinamaanisha kuhisi [nomino mzizi] au kusababisha kuhisi [nomino mzizi]. Kumbuka kuwa maana isiyoelekeza pia inaweza kuonyeshwa kama kirai cha kitenzi kihusishi na kivumishi: sen [nomino mzizi]-do.
- interes(cu) - kuwa/jisikia mwenye hamu (hisi hamu)
interes(gi) - vutia (sababisha kuhisi hamu)
Mi interes(cu) tem basalogi. = Mi sen interesdo tem basalogi.
Ninavutiwa na
isimu.
Basalogi interes(gi) mi.
Isimu inanivutia.
- pilo(cu) - kuwa/jisikia mchovu (hisi uchovu)
pilo(gi) - chosha (sababisha kuhisi uchovu)
Te pilo(cu). = Te sen pilodo.
Amechoka/anajisikia mchovu.
Tesu ergo pilo(gi) te.
Kazi yake inamchosha.
Kiambishi awali xor- kinaweza kutumika na vitenzi vya hisia kuonyesha tofauti ifuatayo:
Mi le interes tem basalogi lefe multi nyan.
Nilikuwa na hamu na isimu miaka mingi iliyopita.
Te le pilo dur na ergo.
Alikuwa amechoka wakati akifanya kazi.
dhidi ya:
Mi le xorinteres tem basalogi lefe multi nyan.
Nilianza kupendezwa na isimu miaka mingi
iliyopita.
Te le xorpilo dur na ergo.
Alichoka/alianza kuchoka wakati akifanya kazi.
Vitenzi vya Hali
Vitenzi elekezi na sielekezi vya hali vinafanana na vitenzi vya hisia. Ni nomino za hali ambazo zinaweza kutumika kama vitenzi elekezi na sielekezi zikimaanisha kuwa na [mzizi wa nomino] au kusababisha kuwa na [mzizi wa nomino]. Kumbuka kuwa maana isiyoelekeza pia inaweza kuonyeshwa kama kirai cha kitenzi kihusishi na kivumishi: sen [mzizi wa nomino]-pul.
- termo(cu) - kuwa moto/joto (kuwa na joto)
termo(gi) - tia joto (sababisha kuwa na joto)
Misu kafe no haji termo. = Misu kafe no haji sen termopul.
Kahawa yangu si
moto tena.
Kam yu le termo banyo-kamer?
Je, ulipasha joto bafuni?
- cinon(cu) - kuwa na akili (kuwa na akili)
cinon(gi) - tia akili (sababisha kuwa na akili)
Syensiyen cinon. = Syensiyen sen cinonpul.
Mwanasayansi ana akili.
Eskol le cinon te.
Shule ilimfanya awe na akili.
- talento(cu) - kuwa na kipaji (kuwa na kipaji)
talento(gi) - fanya awe na talanta/toa kipaji(sababisha kuwa na talanta)
Lalayen talento. = Lalayen sen talentopul.
Mwimbaji ana kipaji.
Patre le talento lalayen.
Baba alimpa mwimbaji kipawa.
Kiambishi awali xor- kinaweza kutumika pamoja na vitenzi vya hali kuashiria ufuatao.
Jaledin le termo. = Jaledin le sen termopul.
Jana kulikuwa na joto.
To le xortermo fe midinuru. = To le xorsen/sencu termopul fe midinuru.
Ilianza kuwa joto/ ikawa na joto saa sita mchana.
Vitenzi Visivyo na Mtendaji
Katika maana isiyoelekeza ya vitenzi elekezi na sielekezi visivyo na mtendaji, kitendo ni kitu kinachomtokea kiima badala ya kitu ambacho kiima hukifanya.
- kasiru(cu) - vunjika (vunjika)
kasiru(gi) - vunja (sababisha kuvunjika)
Janela le kasiru(cu).
Dirisha lilivunjika.
Mi le kasiru(gi) janela.
Nilivunja dirisha.
- boyle(cu) - chemka (chemshwa)
boyle(gi) - chemsha (sababisha kuchemka)
Sui le boyle(cu).
Maji yalichemka.
Te le boyle(gi) sui.
Alichemsha maji.
- fini(cu) - isha (fikia mwisho)
fini(gi) - maliza, komesha (sababisha kufikia mwisho)
Jange le fini(cu).
Vita viliisha.
Ete le fini(gi) jange.
Walimaliza vita.
Vitenzi vya Mkao/Mahali au Mwendo
Katika maana isiyoelekeza ya vitenzi elekezi na sielekezi vya mkao/mahali au mwendo kiima ni mtendaji na mtendewa.
- esto(cu) - simama (simama)
esto(gi) - simamisha (fanya kusimama au sababisha kusimama)
Am esto(cu)!
Simama!
Am esto(gi) mobil!
Simamisha gari!
- harka(cu) - songa (fanya mwendo)
harka(gi) - sogeza (sababisha kusonga)
Am no harka(cu)!
Usisogee!
Mi le harka(gi) yusu kursi.
Nilisogeza kiti chako.
- buka(cu) - funguka (kuwa wazi)
buka(gi) - fungua (fanya wazi)
Dwer le buka(cu).
Mlango ulifunguka.
Mi le buka(gi) dwer.
Nilifungua mlango.
Katika unyambulishaji wa maneno, vitenzi elekezi na sielekezi hufanya kazi kama vitenzi elekezi bila hitaji la -gi. Hata hivyo, wakati maana isiyoelekeza ya kitenzi inahitajika katika unyambulishaji wa maneno, -cu lazima itumike. Linganisha vivumishi vifuatavyo vilivyonyambuliwa na buka na kiambishi tamati -ne:
bukane merasem - sherehe ya ufunguzi
bukacune dwer - mlango unaofunguka
Vivumishi/Vielezi
Katika Globasa, vivumishi na vielezi vinavyofafanua vitenzi vina umbo sawa.
- bon - zuri, vizuri
- velosi - haraka, upesi
- multi - nyingi, -ingi
Vivumishi/vielezi hutangulia nomino/vitenzi vinavyovifafanua.
Hinto sen bon yam.
Huu ni chakula kizuri.
Bebe bon yam.
Mtoto anakula vizuri.
Uma velosi pawbu.
Farasi anakimbia haraka.
Vinginevyo, vielezi vinaweza kuonekana baada ya kitenzi, lakini kabla ya yambwa tendewa na yambwa tendeshi, ikiwa zipo: Kiima - Kitenzi - (Yambwa Tendewa na Yambwa Tendeshi) - Kielezi.
Bebe yam bon.
Mtoto anakula vizuri.
Bwaw glu sui velosi.
Mbwa anakunywa maji haraka.
Vielezi pia vinaweza kuhamishiwa mwanzoni mwa sentensi, mradi tu kuna kituo dhahiri chenye mkato ili kutenganisha kirai na sehemu nyingine ya sentensi. Bila kituo, kivumishi/kielezi kinaweza kutafsiriwa kimakosa kama kinafafanua kiima.
Velosi, bwaw glu sui.
Haraka, mbwa anakunywa maji.
Unyum, te le idi cel banko.
Kwanza, alienda benki.
Vivumishi/Vielezi katika Vishazi vya Mwanzo wa Sentensi
Yafuatayo ni vivumishi/vielezi vinavyotumika sana katika vishazi vya mwanzo wa sentensi vikifuatwa na kituo dhahiri kabla ya sehemu nyingine ya sentensi.
- Ripul, Rili, Rimarali, - Tena
- Dumarali, - Wakati mwingine
- Pimpan, - Mara nyingi
- Ible, - Labda
- Maxpul, - Zaidi ya hayo
- Pia, - Pia
- Abruto, - Ghafla
- Total, - Kabisa
- Yakin, - Hakika
- Ideal, - Kikamilifu
- Mimbay, - Bila shaka
- Mingu, - Kwa uwazi
- Sipul, - Hakika
- Fori, - Mara moja
- Sati, - Kweli
- Umumi, - Kwa ujumla
- Nerleli, - Hivi karibuni
- Telileli, - Muda mrefu uliopita
- Nerxali, - Karibuni
- Telixali, - Baada ya muda mrefu
Ulinganisho wa Vivumishi/Vielezi
Ulinganisho wa vivumishi/vielezi huonyeshwa kama ifuatavyo kwa kutumia maneno maxmo (zaidi, -enye zaidi), minmo (chini ya), denmo (kama),kom (kama, kuliko).
- maxmo kimapul kom... - ghali zaidi kuliko...
- minmo kimapul kom... - nafuu kuliko...
- denmo kimapul kom... - ghali kama...
Ili kuonyesha -enye zaidi (-st) na -enye uchache zaidi, Globasa hutumia maxim... te/to na minim... te/to. Neno of linamaanisha kati ya au nje ya. Kumbuka kwamba viwakilishi te/to lazima vifuate kivumishi mara moja kwani vishazi nomino lazima viishie na nomino au ki wakilishi. Tazama Vishazi Nomino.
- maxim juni te (of misu bete) - mdogo zaidi (wa watoto wangu)
- minim kimapul to (of yusu mobil) - nafuu zaidi/gharama ndogo zaidi (ya magari yako)
Ili kuonyesha kadiri... ndivyo..., Globasa hutumia folki maxmo/minmo, maxmo/minmo.
- folki (to sen) maxmo neo, (to sen) maxmo bon - kadiri (kilivyo) kipya zaidi, (ndivyo kilivyo) bora zaidi
Maneno ya Kitenzi/Kivumishi-Kielezi
Kando na maneno ya nomino/kitenzi na maneno ya kivumishi/kielezi, Globasa ina aina ya tatu ya maneno: maneno ya kitenzi/kivumishi-kielezi. Vitenzi visaidizi pekee ndivyo vipo katika aina hii ambayo ina maneno matatu tu: abil, musi na ingay.
- abil: (kitenzi) weza; (kivumishi/kielezi) -enye uwezo, inayoweza
- musi: (kitenzi) lazima; (kivumishi/kielezi) ambayo lazima, ambayo inabidi
- ingay: (kitenzi) inafaa, inapaswa; (kivumishi/kielezi) inayofaa, inayo paswa
Viambishi Vya Kawaida
Kiambishi Tamati Cha Nomino -ya
Kiambishi tamati -ya kina kazi mbalimbali muhimu na ni sawa na viambishi tamati kadhaa vya Kiingereza: -ity, -ness, -dom, -hood, -ship.
- Nomino dhahania hunyambuliwa kutoka kwa vivumishi/vielezi kwa kuongeza -ya.
-
real - halisi (kivumishi)
realya - uhalisi (nomino) -
bimar - -gonjwa, -a kuumwa (kivumishi)
bimarya - ugonjwa (nomino) -
huru - huru (kivumishi)
huruya - uhuru (nomino) -
solo - peke yake (kivumishi)
soloya - upweke (nomino)
- Kiambishi tamati -ya hutumiwa kunyambua nomino dhahania na nomino zisizohesabika kutoka kwa aina mbalimbali za nomino za dhahiri na zinazohesabika.
- poema - shairi (nomino dhahiri)
- poemaya - ushairi (nomino dhahania)
Kiambishi tamati -ya kinamaanisha -hood au -ship kinaposhikamanishwa na nomino zinazoashiria mahusiano.
-
matre - mama (nomino dhahiri)
matreya - umama (nomino dhahania) -
patre - baba (nomino dhahiri)
patreya - ubaba (nomino dhahania) -
doste - rafiki (nomino dhahiri)
dosteya - urafiki (nomino dhahania)
Katika baadhi ya matukio nomino dhahiri au inayohesabika hutumiwa kama kitenzi na nomino dhahania au isiyohesabika hunyambuliwa kwa kutumia -ya na kufanya kazi kama mwenzake wa kitenzi.
-
imaje - taswira/picha (nomino dhahiri), taswira/fikiria (kitenzi)
imajeya - mawazo (nomino dhahania) -
turi - safari (nomino inayohesabika), safiri (kitenzi)
turiya - utalii (nomino isiyohesabika)
Vile vile, sehemu za mwili zinazohusishwa na hisi tano huashiria kitendo husika (kitenzi), huku -ya ikitumika kunyambua nomino dhahania.
-
oko - jicho (nomino dhahiri), ona, tazama (kitenzi)
okoya - utazamaji, kuona au hisia ya kuona (nomino dhahania) -
ore - sikio (nomino dhahiri), sikia (kitenzi)
oreya - usikivu au hisia ya kusikia (nomino dhahania) -
nasa - pua (nomino dhahiri), nusa (kitenzi)
nasaya - unukaji au hisia ya kunusa (nomino dhahania) -
xeto - ulimi (nomino dhahiri), onja (kitenzi)
xetoya - ladha au hisi ya ladha (nomino dhahania) -
pifu - ngozi (nomino dhahiri), gusa (kitenzi)
pifuya - mguso au hisia ya mguso (nomino dhahania)
-
Vihusishi hubadilishwa kuwa nomino/vitenzi kwa kutumia kiambishi tamati -ya. Tazama Vitenzi vya Vihusishi.
-
Kiambishi tamati -ya pia hutumiwa kubadilisha maneno mengine ya kazi kuwa nomino. Tazama Maneno ya Kazi.
Asili ya neno -ya: Kihindi (सत्य "satya" - ukweli), Kihispania (alegría - furaha)
Kiambishi Awali du-
Globasa hutumia kiambishi awali du- kuelezea jina-kitenzi (gerund).
- dudanse - (kitendo cha) kucheza dansi
- dulala - (kitendo cha) kuimba
Kiambishi awali du- pia hutumika kwa wakati endelevu/tabia wa kitenzi. Tazama Aina za Vitenzi.
Kiambishi awali du- kimekatwa kutoka kwa neno dure (muda).
Asili ya neno
dure: Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kihispania
Kiambishi Tamati cha Nomino/Vitenzi -gi
Kiambishi tamati -gi kinaweza kutumika kwa vivumishi, nomino na vitenzi.
Vivumishi
Kiambishi tamati -gi hubadilisha vivumishi kuwa vitenzi elekezi.
-
bala - -enye nguvu
balagi - imarisha -
pul - -mejaa
pulgi - jaza -
mor - -liokufa
morgi - ua
Nomino
Kiambishi tamati -gi humaanisha sababisha kuwa kinapoongezwa kwenye nomino.
-
zombi - zombi
zombigi - badili kuwa zombi -
korbani - mwathiriwa
korbanigi - fanya mwathiriwa, dhulumu
Vitenzi
Kiambishi tamati -gi pia hutumika kubadili vitenzi sielekezi na vitenzi elekezi kuwa vitenzi visababishi, au hutumika kwa hiari katika vitenzi elekezi na sielekezi, kama inavyoonekana chini ya Aina za Vitenzi hapo juu.
Kiambishi tamati -gi kimefupishwa kutoka gibe (toa).
Asili ya neno
gibe: Kiingereza (give), Kijerumani (geben, gibt) na Kimandarini (给 “gěi”)
Kiambishi Tamati cha Nomino/Vitenzi -cu
Kiambishi tamati -cu kinaweza kutumika kwa vivumishi na nomino, pamoja na vitenzi, kama inavyoonekana chini ya Aina za Vitenzi hapo juu.
Vivumishi
Kiambishi tamati -cu (pata/kuwa) hubadilisha vivumishi kuwa vitenzi visivyoelekeza.
-
roso - nyekundu
rosocu - kuwa mwekundu (pata wekundu) -
mor - -liokufa
morcu - kufa (kuwa mfu)
Nomino
Kiambishi tamati -cu kinamaanisha kuwa kinapoongezwa kwa nomino.
-
zombi - zombi
zombicu - geuka kuwa zombi -
ixu - mtu mzima
ixucu - kuwa mtu mzima, kufikia umri
Kiambishi tamati -cu kimefupishwa kutoka cudu (chukua, pata, miliki,
tunukiwa)
Asili ya neno cudu: Kimandarini (取得 "qǔdé"), Kikorea (취득 “chwideug”)
Kiambishi Tamati cha Kivumishi/Kielezi -li
Katika Globasa, vivumishi/vielezi hunyambuliwa kutoka kwa nomino kwa kutumia viambishi tamati mbalimbali. Tazama orodha kamili ya viambishi tamati chini ya Uundaji wa Maneno. Mojawapo ya kawaida zaidi ni kiambishi tamati -li (ya, inayohusiana na).
-
musika - muziki
musikali - -a kimuziki, kimuziki -
denta - jino
dentali - -a meno -
dongu - mashariki
donguli - -a mashariki -
Franse - Ufaransa
Franseli - -a Kifaransa
Kiambishi tamati -li pia hutumika kunyambua vivumishi/vielezi kutoka kwa maneno ya kazi. Tazama Maneno ya Kazi.
Asili ya neno -li: Kifaransa (-el, -elle), Kihispania (-al), Kiingereza (-al, -ly), Kijerumani (-lich), Kirusi (-ельный “-elni”, -альный “-alni”), Kituruki (-li)
Kiambishi Tamati cha Kivumishi/Kielezi -pul
Neno pul linamaanisha -mejaa. Hata hivyo, kama kiambishi tamati -pul humaanisha yenye kiasi cha kutosha au zaidi ya kutosha.
-
humor - ucheshi
humorpul - -enye vichekesho, -a kuchekesha -
hatari - hatari
hataripul - -a hatari
Asili ya neno pul: Kiingereza (full), Kihindi (पूर्ण “purn”), Kirusi (полный “poln-”)
Vivumishi Vitendaji: Kiambishi Tamati -ne
Kiambishi tamati -ne kinamaanisha katika hali tendaji au mchakato wa na hutumiwa kunyambua kile kinachojulikana katika Globasa kama vivumishi tendaji.
Vivumishi tendaji mara nyingi huwa sawa na shiriki tendaji/vitenzi-jina tendaji (present participle) katika Kiingereza (vivumishi vinavyoishia na -ing). Hata hivyo, tofauti na ilivyo kwa Kiingereza, vivumishi tendaji havitumiwi kuunda kauli ya kuendelea/endelevu (Mimi ninalala, Yeye anacheza, n.k.) Badala yake hufanya kazi tu kama vivumishi.
-
somno - lala
somnone meliyen - binti anayelala -
anda - tembea
andane moryen - maiti inayotembea -
danse - cheza
dansene uma - farasi anayecheza -
interes - vutia
interesne kitabu - kitabu kinachovutia -
amusa - burudisha, furahisha
amusane filme - filamu inayoburudisha/ya kufurahisha
Asili ya neno -ne: Kiingereza (-ing), Kifaransa (-ant), Kihispania (-ando), Kijerumani (-en, -ende), Kirusi (-ный “-ny”), Kituruki (-en, -an)
Vivumishi Vitendaji-Mwanzo wa Sentensi
Vivumishi vitendaji vinavyoonekana mwanzoni mwa sentensi vinaweza kuonyeshwa kama vishazi vya kihusishi kwa kutumia aina ya kitenzi kishirikishi.
Doxone, nini le xorsomno.
Akisoma, mtoto alianguka usingizini/alisinzia.
au
Fe na doxo, nini le xorsomno.
Akisoma, mtoto alianguka usingizini.
au
Dur na doxo, nini le xorsomno.
Wakati akisoma, mtoto alianguka usingizini.
Muundo huu ni muhimu hasa wakati kirai kinajumuisha yambwa tendewa kwani, tofauti na shiriki tendaji/vitenzi-jina tendaji katika Kiingereza, vivumishi tendaji katika Globasa haviwezi kufanya kazi kama vitenzi.
Dur na doxo sesu preferido kitabu, nini le xorsomno.
Wakati akisoma kitabu chake anachokipenda, mtoto alianguka usingizini.
Kwa kawaida, virai hivi pia vinaweza kuonyeshwa kama vishazi kamili, kinyume na vishazi vya kihusishi.
Durki te le doxo (sesu preferido kitabu), nini le xorsomno.
Wakati alipokuwa akisoma (kitabu chake anachokipenda), mtoto alianguka usingizini.
Vivumishi Vitendewa
Vivumishi vitendaji vinaweza kufanywa vitendewa kwa kuongeza kiambishi awali tendewa be- ili kunyumbua kile kinachojulikana katika Globasa kama vivumishi vitendaji tendewa (au vivumishi vitendewa kwa ufupi). Hakuna usawa kamili katika Kiswahili kwa vivumishi vitendewa, lakini vinaeleweka vyema kama aina tendewa kamili ya present participle katika Kiingereza.
- belalane melodi - wimbo unaoimbwa au unaoimbwa
- belubine doste - rafiki mpendwa au rafiki anayependwa
Vivumishi Visivyotenda: Kiambishi Tamati -do
Kiambishi tamati -do kinamaanisha katika hali isiyo tendaji ya. Maneno yenye kiambishi tamati hiki yanajulikana katika Globasa kama vivumishi visivyotenda na kwa kawaida hutafsiriwa kama shiriki tendewa/vitenzi-jina tendewa (past participle) katika Kiingereza. Hata hivyo, tofauti na ilivyo kwa Kiingereza, vivumishi visivyotenda havitumiki kuzalisha kauli timilifu au kauli tendewa (Nimefanya kazi, Iliibiwa, n.k.). Badala yake, vinafanya kazi tu kama vivumishi.
Ni muhimu kutambua kwamba, kiufundi, kiambishi tamati -do huongezwa kwenye nomino ya nomino/vitenzi. Kwa sababu hii, -do inaweza kuongezwa kwa elekezi, visivyoelekeza au nomino/vitenzi ambavyo vinaweza kuchukua au kuto kuchukua mtendwa.
Na vitenzi elekezi
- hajado ergo - kazi inayohitajika (katika hali ya lazima)
- bujodo morgiyen - muuaji aliyekamatwa (katika hali ya kukamatwa)
Na vitenzi visivyoelekeza
- Uncudo Nasyonlari - Umoja wa Mataifa (katika hali ya umoja)
- awcudo fleytora - ndege iliyotoweka (katika hali ya kutoweka)
Pamoja na vitenzi vinavyoweza kuwa na/bila mtendwa
- kasirudo janela - dirisha lililovunjika (katika hali ya kuvunjika)
- klosido dwer - mlango uliofungwa (katika hali ya kufungwa)
Asili ya neno -do: Kiingereza (-ed), Kihispania (-ado, -ido)
Kiambishi Tamati cha Kielezi -mo
Vivumishi/vielezi vinavyofafanua vivumishi/vielezi vingine, vinavyojulikana kama vielezi vinavyofafanua vivumishi/vielezi, huongeza kiambishi tamati -mo. Linganisha jozi zifuatazo za vishazi.
-
perfeto blue oko - macho mazuri ya buluu (macho ya buluu ambayo ni mazuri kabisa)
perfetomo blue oko - macho ya buluu kikamilifu (macho ambayo yana rangi ya buluu kikamilifu) -
naturali syahe tofa - nywele nyeusi za asili (sio wigi)
naturalimo syahe tofa - nywele nyeusi kiasili (hazijapakwa rangi) -
sotikal doxone nini - mtoto anayesoma kimya
sotikalmo doxone nini - mtoto anayesoma kimya kimya